Katika mkutano huo, Wanafunzi wa 'Shule ya Msingi Elimu Bora' walipata fursa ya kuwasilisha maonesho mbalimbali ikiwemo burudani za kielimu, usomaji wa Qur’an Tukufu, na maonesho ya uadilifu wa kidini, yote yakiwa ni ushahidi wa ubora wa elimu na malezi wanayopata kupitia taasisi hiyo.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Shule ya Msingi Elimu Bora iliandaa Mkutano na Hafla Maalum kati ya Uongozi wa Shule na Wazazi wa Wanafunzi wa Shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwa mafanikio makubwa siku ya Jumapili, tarehe (4 Mei, 2025 / 1446 Hijria) katika viunga vya shule hiyo, Kipande Na. 31, Block: 1, Vikindu, Vianzi. Mkutano huo ulihudhuriwa na takriban watu 259, wakiwemo wazazi, wageni waalikwa, na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo.
Mgeni rasmi alikuwa: Mkurugenzi Mkuu wa Shule, Maulana Alhaj Sayyid Arif Ali Naqvi, ambaye aliambatana na wageni mashuhuri pamoja na Mkuu wa Masuala ya Kitaaluma wa Shule hiyo.
Katika mkutano huo, wanafunzi wa Shule ya Msingi Elimu Bora walipata fursa ya kuwasilisha maonesho mbalimbali ikiwemo burudani za kielimu, usomaji wa Qur’an Tukufu, na maonesho ya uadilifu wa kidini, yote yakiwa ni ushahidi wa ubora wa elimu na malezi wanayopata kupitia taasisi hiyo.
Akihutubia mkutano huo, Maulana Alhaj Sayyid Arif Ali Naqvi alisisitiza juu ya wajibu mkubwa wa walimu na wafanyakazi katika kuwalea wanafunzi kwa moyo wa uzazi na huruma. Alieleza kuwa malezi bora, yenye misingi ya maadili na elimu, ndiyo njia pekee ya kujenga kizazi kilichoelimika na chenye maadili mema, kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Uongozi wa shule, kupitia msemaji wake Hamim Mgagagi kwa niaba ya Jumuiya ya Hujjatul Asr Society of Tanzania, uliwashukuru wazazi na wageni wote waliohudhuria hafla hiyo, huku ukiwatakia wanafunzi mafanikio mema katika masomo yao na maisha kwa ujumla.
Tumekuwekea hapo chini picha zaidi za hafla hiyo kama ifuatavyo:
Your Comment